Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, awaomba Watanzania kung’amua mtego wa kuliangamiza taifa huku akigongelea msumali dhidi ya yaliyotokea siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 pamoja na siku zilizoendelea.
Amezungumza hayo Jijini Dar es Salaam, Novemba 23,205 wakati akizungumza na waandishi wa habari.
"Nawaomba Watanzania tung'amue mtego wa kuliangamiza taifa letu, tunapita katika kipindi ambacho tukiendekeza uchochezi unaofanywa na watu ambao wapo nje ya nchi na hawaguswi na chochote kuhusu maisha yetu wanaowashawishi vijana wetu kufanya vitendo vya kuumiza nchi yetu tutakaoangamia ni sisi , tutakaoumia kweli ni sisi wenyewe"
"Yaliyotokea tarehe 29 na siku kadhaa zilizofuata tulioumia ni sisi Watanzania wanaoandika habari za uchochezi kupitia mitandao kupitia kwenye vyombo vya habari hawapo Tanzania wanakunywa juisi, wanakula kuku, wanalala vizuri, nchi zao zimetulia, madai yao yanapelekwa kwa mujibu wa taratibu za kisheria na yanafanyiwa kazi na Serikali"-Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.
Chanzo; Tanzania Journal