Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewakamata Pendo John Matongo (19) mkulima mkazi wa Mwembesongo na kumbuka Kwalitaho Barafwa (22) mkulima mkazi wa Mwembesongo kwa tuhuma za mauaji.
Tukio hilo limebainika Novemba 27, 2025 asubuhi katika eneo la mto Morogoro mtaa wa Mchuma Kata ya Kichangani, Manispaa ya Morogoro, ambapo maiti ya mtoto mchanga aitwaye Selina Kumbuka (wiki 3) ilikutwa ikiwa imetupwa na kutelekezwa baada ya kuuawa na wawili hao.
Chanzo; Itv