Jeshi la Polisi nchini, kupitia kwa Msemaji wake wa Polisi (DCP) David Misime, limetoa taarifa kwa vyombo vya habari kwamba taarifa inayoenezwa mitandaoni inayodai kuwa kuanzia Desemba 5 wananchi wasitoke nje kuanzia saa kumi na mbili jioni kwa makundi makundi kutokana na maandamano yanayotarajiwa si ya kweli.
Amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi halijatoa taarifa yeyote ya aina hiyo na kuwa wananchi waipuuze kwa kuwa ni uzushi unaolenga kupotosha umma.
Chanzo; Itv