Kijana aliyefahamika kwa jina la Hassan Shabani (17), mkazi wa Kigamboni, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, amefariki dunia kwa kudaiwa kuchomwa kwa kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake.
Tukio hilo limedaiwa kufanywa na watu ambao hadi sasa hawajajulikana, ambapo mashuhuda wamesema kuwa marehemu alikuwa akikimbia huku akiomba msaada kabla ya kupoteza maisha.
Baba mzazi wa marehemu, Shabani Hasani, amesema alipokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa mke wake akiwa shambani. Kwa upande wake, Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kigamboni, Deogratius Mweli, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Katika hatua nyingine, wananchi wa mtaa huo wametakiwa kushikamana na vyombo vya usalama kukomesha vitendo vya uhalifu, hususan makundi ya vijana wahalifu maarufu kama “dam chafu”
Chanzo; Nipashe