Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Seleman Kizimbani kwa Kumpiga Mkewe

Hamza Omary (38), fundi Selemala na mkazi wa Luchelele, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo ya Mkuyuni, Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, Januari 19, 2026, akikabiliwa na shtaka la kumshambulia mke wake katika Kesi ya Jinai namba 75/2026.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 07, 2026 katika eneo la Luchelele, Mtaa wa Kisoko, majira ya saa 3:30 usiku, ambapo alimshambulia mke wake aitwaye Anna Zacharia kwa kumpiga ngumi, kumrushia sufuria kichwani na kumng’ata mkono wa kushoto.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Mkuyuni, Mhe. Witness Ndosi, Mwendesha Mashtaka Koplo Dorothy Mauma alisema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 240 cha Sura ya 16 ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Marejeo ya mwaka 2023.

“Wewe Hamza Omary unashtakiwa kwa kosa la kumshambulia mke wako aitwaye Anna Zacharia kwa kumpiga, kumrushia sufuria kichwani na kumng’ata mkono wake wa kushoto, na kumsababishia maumivu makali, kitendo ambacho ni kinyume na sheria za nchi,” alisema Mauma.

Hata hivyo, mshtakiwa alikana shtaka hilo na amepelekwa rumande baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana.

Masharti ya dhamana yalikuwa ni kuwa na mdhamini mmoja, barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kata pamoja na fungu la dhamana la ahadi kiasi cha shilingi laki moja (100,000) tu. Mhe. Witness Ndosi ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 02, 2026. 

 

 

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: