Wananchi wa kijiji cha Migombani kata ya Majengo Wilaya ya Monduli mkoani Arusha wamepinga uamuzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) kujenga geti katika kijiji hicho kwa madai kwamba kuwekwa kwa geti hilo kutazuia shughuli za kibinadamu katika kijiji hicho.
Wakizungumza hii leo Januari 21, katika Mkutano wa Kijiji Wananchi hao wamesema kuwa Katika kijiji hicho kuna mipaka halali ya matumizi bora ya ardhi yanayoruhusu kilimo, makazi ya Watu na Utaliii na kuwa sio pori tengefu la wanyama pori.
“Mheshimiwa Mwnyekiti kwa nini tunaikataa TAWA, tuna sababu za msingi na sababu ya kwanza eneo hili la kijiji cha mgombani ni eneo ambalo ni la kilimo na ufugaji lakini pia pamoja na makazi ya Wananchi eneo hili sio tengefu kwa ajili ya Wanyama na ndio sababu ambayo kwanza sisi Wananchi tunaikataa TAWA kwa sababu linapokuwa ni eneo la pori tengefu la Wanyama sisi tunakosa haki ya Kuishi.” Amesema Elibariki John moja ya Wananchi wa Majengo.
Chanzo; Millard Ayo