Watanzania 20 waliokuwa wakifanya kazi nchini Oman wamekwama kurejea nchini baada ya kuacha ajira zao na kukosa fedha za nauli ya kurudi nyumbani.
Baadhi yao, wakizungumza kupitia Global TV kwa njia ya simu kutoka nchini Oman, wameeleza sababu mbalimbali zilizopelekea wao kuacha kazi, zikiwemo mazingira magumu ya kazi, kutolipwa mishahara kwa wakati, pamoja na changamoto za makazi na mikataba ya ajira.
Wamesema hali waliyonayo kwa sasa ni ngumu, huku wakikosa ajira na mahitaji ya msingi, na hivyo kuwaomba Watanzania pamoja na mamlaka husika kuwasaidia ili waweze kurejea salama nchini.
Chanzo; Global Publishers