Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mwanafunzi Afariki Dunia Ikidaiwa Kukatwa na Jembe

Mwanafunzi Kassim Omary (12) wa darasa la sita Shule ya Msingi Bukindwasali, amefariki dunia kwa madai ya kukatwa kichwani na jembe la mwanafunzi mwenzake katika Kata ya Idahina, Tarafa ya Dakama, wilayani Ushetu mkoani Shinyanga.

Tukio hilo limetokea wakati wanafunzi hao wakichimba mchanga kwa ajili ya ukarabati wa darasa uliokuwa ukiendelea shuleni hapo.

Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha tukio hilo ambalo limetokea Januari 21, 2026 na amesema mwanafunzi huyo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Zahanati ya Nyankende.

Kamanda Magomi amedai wakati wanafunzi hao wakiendelea na shughuli hiyo, Kassim alikuwa shimoni na mwenzake James alikuwa akichimba eneo la juu ndipo jembe la James lilipoteleza na kumkata Kassim kichwani. Aidha amesema uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini ukweli wa tukio hilo.

Kamanda Magomi ametoa wito kwa walimu mkoani humo kuwafuatilia wanafunzi wanapokuwa katika kazi za mikono shuleni ili kuzuia majanga kwa yanayozuilika.

 

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: