Baada ya taarifa mtandaoni kusema Mwanamitandao maarufu nchini Tanzania ametekwa na watu wasiojulikana Novemba 21,2025, nyumbani kwake.
Jeshi la Polisi, latoa ufafanuzi juu ya uvumi huo kwa kusema Mwandambo anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za Uchochezi na uchonganishi.
Taarifa hiyo iliyotolewa Novemba 22,2025 inasema “Jeshi la Polisi linamshikilia Mwalimu Clemence Mwandambo kwa tuhuma za uchochezi.”
Ambapo Mwandambo, alikamatwa Novemba 22,2025, Asubuhi maeneo ya Uzunguni, Mbeya akitoa na kusambaza maneno ya uchochezi na uchonganishi kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii facebook na instagram.
Chanzo; Tanzania Journal