Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Watumia Ushirikina Kukwamisha Miradi Waonywa

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida kimewaonya baadhi ya wananchi wanaotumia imani za kishirikina kukwamisha miradi ya uchimbaji wa visima vya maji.

Kimesema hali hiyo inachangia kuendelea kwa changamoto ya uhaba wa maji katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Katibu wa CCM Wilaya ya Singida Vijijini, Hanzuruni Mtebwa, ametoa onyo hilo baada ya wataalamu wa maji kufika katika kitongoji cha Gairu, Kijiji cha Sagara, kwa ajili ya kuchimba kisima cha maji, ili kupunguza adha ya ukosefu wa maji kwa wakazi wa eneo hilo.

Mtebwa amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi kuzuia utekelezaji wa miradi kwa njia za kishirikina, licha ya wataalamu kuthibitisha uwepo wa maji katika maeneo husika.

Mtebwa amesema: “Kuna tabia moja naomba tuiache. Wataalamu wanafika kuchimba kisima, maji hayapatikani licha ya vipimo kuonesha maji yapo, eti kwa sababu kuna mzee mmoja hajamuomba ruhusa. Acheni mchezo huu. Wewe mmoja nani hadi ukwamisha maendeleo ya watu wengi".

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: