Rais mstaafu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania awamu ya nne na mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, amemuomba Makamu wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuongezewa ardhi ya kutosha kwenye chuo kikuu cha Dar es Salam Kampasi ya Kagera kwa mahitaji ya sasa na siku zijazo
Chuo kikuu cha Dar es salaam kampasi ya Kagera kinajengwa katika wilaya ya Bukoba mkoani kagera kata Karabagaine chenye ukubwa wa ardhi yenye hekari zaidi ya miamoja ambazo zimetolewa bure na wanakijiji wa Itahwa na Kangabusharo katika kata hiyo kwa kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu nchini
Dkt Kikwete ametoa ombi hilo baada ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kampasi ya chuo hicho kinachojengwa kwa mkopo wa mashart nafuu kutoka benki ya dunia kwa thamani ya sh bilioni 14 ikiwa ni matayarisho ya utekelezaji wa wa mradi wa elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi Tanzania
Makamu wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzani Mhe Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi amesema maombi hayo wanayafanyia kazi huku akiiagiza wizara ya ujenzi pamoja na wizara ya elimu sayansi na Tecknologia kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha taratibu na mahitaji mengine ya muhimu kuandaliwa mapema ili kuwezesha chuo kikuu cha Dar es salam kampasi ya Kagera kuanza bila vikwazo.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amemshukuru Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea chuo hicho ambacho kinachotarajiwa kufunguliwa mwanzoni mwa mwaka ujao (2026) na kitaanza kubeba wanachuo zaidi ya 800 na kufikia wanachuo zaidi ya elf moja ifikapo 2030.
Chanzo; Clouds Media