Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Tamthilia Chanzo Wauguzi Kusimamishwa Kazi

Wizara ya Afya Zanzibar imewasimamisha kazi Wauguzi wawili kupisha uchunguzi wa kisa cha mtoto Said Abdallah Khamis mwenye umri wa Miezi 4 ambaye alifikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Lukumba Mjini Unguja baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitali hapo akiwa na tatizo la tumbo wakati akipatiwa matibabu ilipelekea kupata tatizo la kuvimba mkono.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Mngereza Miraji ambapo amesema Wauguzi hao wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi utakaohusisha mabaraza ya wauguzi ambayo yatachunguza kwa kina madai mbalimbali yaliotolewa na familia ya kuwa wauguzi hao walihusika na kupelekea changamoto hiyo.

Aidha Ndugu wa familia wamewalalamikia wauguzi wawili ambao wamesimamishwa kazi kwa kudaiwa kufanya uzembe baada ya mama mlezi wa mtoto kuwaambia mkono ulianza kuvimba na kubadilika rangi ambapo mama huyo ameeleza wakati akiwaambia wauguzi hali ya mtoto wake walikua wakitazama na wengine wakiwa wanachezea Kompyuta na kupuuzia.

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: