Mzee mwenye umri wa miaka 60 anayeishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa amewasilisha malalamiko yake kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akidai kuibiwa mtoto mmoja wa kiume baada ya mke wake kujifungua mapacha katika Hospitali ya Wilaya ya Nkasi.
Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu wakati wa mkutano wa hadhara, mzee huyo amesema tukio hilo lilitokea baada ya mke wake kujifungua mapacha hospitalini hapo, ambapo baadaye walikabidhiwa mtoto mmoja pekee.
Amesema kwa muda mrefu amekuwa akifuatilia suala hilo bila kupata majibu ya kuridhisha, hivyo kumuomba Waziri Mkuu kuingilia kati ili haki ipatikane na ukweli wa tukio hilo ujulikane.
Chanzo; Eatv