Wananchi wa Mtaa wa Elkiroa Kata ya Daraja Mbili Mkoani Arusha wameingilia kati sakata la mwanamke aitwaye Jesca Godgrey (23) la kupigwa na kufanyiwa ukatili na mume wake mara kadhaa kutokana na kuchelewa kupika pamoja na kulazimishwa kufanya tendo la ndoa huku akiwa na watoto wadogo watatu ambao amewapata ndani ya mwaka mmoja na miezi mitatu.
Akizungumza na AyoTV Jesca ameeleza kwa kina chanzo cha kupigwa ni kutokana na kuchelewa kupika na alivyojifungua mtoto mdogo mwanaume huyo alikuwa akitaka tendo la ndoa na baada ya kukataa kutokana na madhara aliyoyapata hapo awali ndipo mwanaume huyo alipoanza kumpiga.
“Mapacha wa kiume na kike ndio ulikuwa uzao wangu wa kwanza na wale mapacha wakiwa na miezi mitatu nilikuwa tulifanya bila kupangilia na ndipo niliskilia mtoto anacheza tumboni nikaenda kupima nikaambiwa nina ujauzito wa miezi minne nikawa naishi hivyo hivyo kwa shida navumilia siku ziende na watoto nikiangalia watoto ni wadgo ujauzito huu nimeangaika nao mpaka najufungua nimesaidiwa gharama na shemeji yangu yeye ajachangia chochote.” Amesema Jesca.
Chanzo; Millard Ayo