Ni huzuni kwa wakazi wa kitongoji cha mpakani kata ya Ijombe halmashauri ya wilaya ya Mbeya wakiomboleza kifo cha kijana Ndele Mwananginga aliye fariki dunia baada ya kuchomwa na kisu na kaka yake, akiamulia ugomvi ulio muhusisha kaka yake.
Ndugu na majirani wa familia hiyo wanaeleza masikitiko yao juu ya kifo hicho kinachodaiwa kua ni kisa cha kwanza kutokea kwenye kitongoji chao kiki husisha ndugu wawili wa familia moja.
Ambius Aron ni mwenyekiti wa Serikali ya kitongoji cha Mpakani anaeleza tukio hilo lilivyo tokea ambapo marehemu alipigiwa simu usiku ikimtaarifu kuwa kaka yake kuanzisha vurugu kwenye kilabu cha pombe ndipo akaenda kwaajili ya kuamulia na kumchukua ndugu yake.
Chanzo; Wasafi