Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema kuwa watu wanaosafiri kwenda mikoani ni jambo la kawaida linalotokea kila mwaka, na si kitu cha kushangaza au kuhusishwa na sababu nyingine.
“Naomba niwaambie kitu kimoja: kama kweli kuna adui, atakuwa amefanikiwa endapo atagundua kuwa tumeingiwa na woga. Woga ni janga kubwa; akikutisha ukatishika,” alisema Chalamila.
Akaongeza: “Ndio maana Rais amesema kwamba kwa namna yoyote ile tutaendelea kulilinda taifa letu.”
Chanzo; Bongo 5