Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema viongozi wake wamezuiwa kumwona mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu aliyepo katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Lissu yupo mahabusu kwa kesi ya uhaini inayomkabili kwa takriban miezi minane sasa, tangu alipokamatwa Aprili 2025, akiwa mkoani Ruvuma kwa ziara ya chama hicho.
Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Magereza, Elizabeth Mbezi amesema hana taarifa iwapo kuna zuio la viongozi wa Chadema kumwona Lissu.
Taarifa ya kuzuiwa kumwona kiongozi huyo, imetolewa leo, Jumapili Novemba 30, 2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Brenda Rupia.
Brenda kupitia taarifa hiyo, amesema viongozi hao wamezuiwa kuingia katika gereza hilo siku za karibuni walipokwenda kumuona kiongozi wao huyo.
Chanzo; Mwananchi