Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Manyara zimeharibu zaidi ya hekta 10,000 za mashamba ya mahindi na maharage katika Kata ya Naisinyai, wilayani Simanjiro, huku maji yakisomba baadhi ya mazao na kuzingira nyumba za wakazi katika maeneo hayo.
Athari za mvua hizo zimekumba pia kata za Mirerani, Shambarai na Endiamtu, ambapo mashamba mengi yameharibiwa na maji kuanza kuingia katika baadhi ya makazi ya wananchi.
Hali hiyo imeibua hofu kwa wakazi wa maeneo hayo, huku wakiiomba Serikali na wadau mbalimbali kuchukua hatua za haraka ili kudhibiti madhara ya mafuriko na kuwasaidia wananchi waliopoteza mazao yao.
Chanzo; Global Publishers