Naibu Waziri wa TAMISEMI Reuben Kwagilwa ametoa maelekezo kwa Watumishi wote waliopo chini ya Wizara ya TAMISEMI kuzingatia muda sahihi wa kufika kazini.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo katika Shule ya msingi Kisasa Jijini Dodoma, ambapo ametoa maelekezo kwa Walimu pamoja na Wakuu wa Shule zote Nchini kuzingatia kanuni za kudumu za watumishi wa umma.
“ Mimi nimefika hapa saa moja na nusu asubuhi, nimekuwa Mtu wa tano kusaini kitabu cha Watumishi, hapa kuna takribani Watumishi mia na tano (105) , lakini wanaozingatia muda wa kufika kazini ni 15,
“Natoa maelekezo Nchi nzima kwa niaba ya Waziri wa Tamisemi, Watumishi waliopo chini ya Wizara yetu wazingatie muda wa kufika kazini Kama ilivyopangwa, Lengo tunataka Watanzania wahudumiwe, Wasikilizwe na hili Ndio leongo la Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan”, Amesema Kwagilwa
Chanzo; Clouds Media