Kijana mmoja aitwaye Tatu Mgeta (23) amefariki dunia leo Januari 20, 2026, baada ya kugongwa na treni ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka Tabora kuelekea Mpanda.
Tukio hilo limetokea asubuhi katika eneo la Isevya, wakati marehemu akijaribu kuvuka reli akiwa amepanda pikipiki aina ya bodaboda.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tabora, Omary Simba, amesema kuwa mtu mmoja amejeruhiwa katika ajali hiyo na tayari amekimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Kwa upande wake, muongoza treni Emmanuel Mtiku amesema kuwa kuna utaratibu wa kuonyesha bendera nyekundu kabla ya treni kupita ili kutoa tahadhari kwa watumiaji wa barabara. Amewataka wananchi kuzingatia alama na taratibu za usalama wanapokuwa karibu na reli ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika.
Chanzo; Global Publishers