Viongozi wawili wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu na Moza Ally, wamepata ajali baada ya gari walilokuwa wakisafiria, Toyota Prado lenye namba za usajili, T847 DKR, kugongwa kwa nyuma na gari aina ya Subaru Forester lenye namba za usajili T491 EGT.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, ajali hiyo ilitokea usiku wa jana, Januari 20, 2026 majira ya saa 5:20 katika eneo la Morocco, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Chanzo; Global Publishers