Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Butiku Asema Kufungia Makanisa Haikuwa Sawa

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mwalimu Nyerere Foundation Mzee Joseph Butiku, amesema kitendo cha Serikali kufungia Kanisa la Gwajima hakikuwa sawa na kusema kama Gwajima alikosea angepelekwa yeye Mahakamani na sio kuwaadhibu Waumini wote.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo January 19,2026, Mzee Butiku amesema “Tukienda na mifano mingine akina Gwajima, am sorry Mimi siisemi Serikali, Mimi nasema tabia yetu tu, rule of law, Gwajima alikuwa na Wanachama wangapi?, kamata Gwajima mpeleke Mahakamani ajibu tuhuma zake lakini huwezi kufunga Makanisa ambayo Watu wote wanakwenda kushughulikia imani zao”

“Maandamano haya ni mambo ya kawaida Watu wengine wapo huko wanaandamana ilimradi yawe ya amani lakini hapa kila wakati maandamano, Polisi wanasema ooh Polisi ina intelejensia wakiandamana, si muache waandamane wavunje nyumba za Watu tuone hawa Watu kumbe Wakorofi, kwanini unawatetea wakati wote unawasaidia kuficha ubaya wao, ngoja watoke tuone hawa Watu wa hovyo kumbe tukiwaruhusu maandamano wanakwenda kuiba”

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: