Baraka Melami (40), mkazi wa Kijiji cha Olevolosi, Kata ya Kimnyaki wilayani Arumeru mkoani Arusha ambaye anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Selian baada ya kujeruhiwa kwa kukatwa uume na mkewe, Anna Melami (30).
Hata hivyo Melani amemsamehe mkewe huyo.
Akizungumza na Mwananchi leo Novemba 26,2025 hospitalini hapo, Melami mbali na kuomba msaada wa gharama za matibabu amesema kuwa amemsamehe mkewe kwa tukio alilolifanya akiomba mkewe aachiwe huru.
“Hali yangu siyo nzuri sana ninaomba Watanzania wanisaidie kulipa gharama za matibabu, wanishike mkono ili niweze kulipa kwani nimeambiwa hadi jana gharama ni zaidi ya Sh1.5 milioni,”amesema Melami.
Akizungumzia tukio hilo Melami amesema walifunga duka na kurudi nyumbani bila kuwa na ugomvi wowote.
“Kwa kuwa kulikuwa na baridi nilikuwa nimelala na suruali, mwenzangu akaja kunipapasa kama anataka tufanye tendo la ndoa, lakini iliposimama akaikata yote kuanza chini kabisa,”amesema.
Chanzo; Mwananchi