Mbunge wa Jimbo la Kwahani, Zanzibar, Mkoa wa Mjini, Mohammed Abdallah Makame (Laki), leo Novemba 23 ametembelea Jimbo la Kwahani kwa mara ya kwanza tangu aapishwe kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Laki amefanya ziara ya kuwatembelea wananchi wa jimbo hilo, huku akiwakumbusha kuhusu vipaumbele alivyowaahidi wakati akiomba ridhaa ya kuwaongoza.
Mbunge huyo ametumia nafasi hiyo kufafanua kilichotokea bungeni wakati wa kuapishwa, ambapo alionekana kubabaika na kupata kigugumizi wakati wa kuapa.
Amesema bado hajajua nini kilitokea, kwani tayari ameshawahi kuapa mara kadhaa akiwa diwani na pia amewahi kuwasilisha ripoti mbalimbali katika shughuli zake za kisiasa ndani ya chama na maeneo mengine.
Chanzo; Global Publishers