Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ametaka kuzingatiwa kwa maoni yaliyotolewa na waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuhusu uchaguzi.
Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho iliyomnukuu mwenyekiti wao huyo ambaye yuko gerezani Ukonga kutokana na mashtaka ya uhaini yanayomkabili, Lissu anaunga mkono taarifa zilizotolewa na waangalizi hao wa uchaguzi akisema zimeonesha uhalisia wa hali ilivyokuwa kabla, baada na wakati wa uchaguzi.
Katika taarifa ya SADC ilisema kuwa uchaguzi wa Tanzania uliofanyika Oktoba 29, kuwa haukukidhi viwango vya kidemokrasia vilivyowekwa na jumuiya hiyo taarifa ambayo iliungwa mkono na ile ya AU.
Chanzo; Nipashe