Mtoto wa miaka miwili, Ibrahimu Athumani, amefariki dunia huku kaka yake wa miaka mitano akijeruhiwa vibaya baada ya moto kuteketeza nyumba yao katika kijiji cha Kinkwembe, Wilayani Kilindi. Tukio hilo limetokea wakati baba mzazi akiwa shambani, ambapo Ibrahimu alifariki akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Handeni, huku majeraha makubwa aliyopata mtoto wa miaka mitano yakisababisha apewe rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Bombo jijini Tanga kwa matibabu zaidi.
Mamia ya wananchi wamejitokeza kuifariji familia hiyo huku viongozi wa kijiji na Diwani wa Kata ya Mkindi, Mhe. Hilali Msigwa, wakielezea hatua za awali zilizochukuliwa kufuatia janga hilo. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Handeni amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kueleza kuwa hali ya majeruhi ilihitaji uangalizi wa kibobezi zaidi, jambo lililopelekea kupelekwa Bombo huku simanzi kubwa ikiendelea kutanda kijijini hapo.
Chanzo; Itv