Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesisitiza kuwa Vyuo Vikuu vinavyojenga kampasi mpya katika maeneo mbalimbali nchini kuhakikisha kampasi hizo zinajikita katika kutoa mafunzo ya ujuzi (Amali).
Agizo hilo limetolewa jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, wakati wa kikao kazi cha kimkakati kati ya Wizara na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara.
Prof. Mkenda amesema "Haya ni utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 inayosisitiza kuandaa wahitimu wenye ujuzi hivyo hakikisheni kampasi hizi mpya zinatoa mafunzo ya amali yaani ufundi na ufundi stadi msitoke katika malengo haya."
Chanzo; Bongo 5