Baadhi ya ndugu wa watuhumiwa wanaokabiliwa na kesi ya uhaini, wamefurika katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, wengine wakiwa na maua, kusubiri ndugu zao waachiwe.
Idadi kubwa ya watuhumiwa hao, waliachiwa hapo jana kufuatia agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kutaka walioshiriki kwenye maandamano ya Oktoba 29, 2025 waachiliwe.
Jambo hilo limewapa nguvu baadhi ya ndugu ambao wanatarajia ndugu zao wanaweza kuachiwa huru leo.
Chanzo; Global Publishers