“Unazungumzia Congo iliyovurugika miaka 30 iliyopita na haijapata amani mpaka leo. Wewe unayefikiria kuivuruga nchi yako ya Tanzania leo, utakaa miaka 30 bila kuiona amani. Kama wewe ni kijana leo, utakaa miaka 30 hujaiona, kwa sababu hiyo si njia rahisi; njia rahisi ni mazungumzo.” alisema Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene
Ametoa kauli hiyo wakati wa Mkutano wa Pili unaohusisha
Pande Tatu ikiwemo Serikali ya Tanzania, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani UNHCR ambapo pia walitumia mkutano huo kusaini nyaraka zinazoelezea Mpango wa Urejeshwaji wa Wakimbizi Elfu Themanini na Sita na Mia Mbili Hamsini na Sita waliopo hapa nchini.
Chanzo; Bongo 5