Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la James Francis mwenye umri wa miaka 28 anayeishi wilayani Babati mkoani Manyara ameuawa kikatili kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Hayo yamejiri Wilaya ya Babati, ambapo na mtuhumiwa anayetajwa kwa jina la Eliasa Said anadaiwa kumshambulia James anayedaiwa kuwa mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mmoja aitwaye Melania Khuway ambaye pia anadaiwa kuwa mpenzi wa Eliasa.
Marehemu James Francis anadaiwa kuwa alikuwa ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara.
Chanzo; Itv