Imeelezwa kwamba ugonjwa wa moyo ndiyo chanzo cha kifo cha aliyekuwa mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama ambaye alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Bunge, Baraka Leornad leo wakati akisoma wasifu wa marehemu Jenista, baada ya ibada ya misa iliyofanyika katika Kanisa la Maria-Theresa Ledochowska, Parokia ya Kiwanja cha Ndege, Jimbo Kuu Katoliki Dodoma.
“Jenista Mhagama alifariki dunia Desemba 11, 2025 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma kwa maradhi ya moyo,” amesema Leonard.
Marehemu Jenista atazikwa Jumanne ya Desemba 16, 2025 katika Kijiji cha Ruanda, Mbinga mkoani Ruvuma
Chanzo; Nipashe