Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mwalimu Nyerere Foundation, Mzee Joseph Butiku, amesema hana taarifa zozote kuhusu alipo aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi na Cuba, Humphrey Polepole, tofauti na taarifa zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa huenda anafahamu alipo au kilichompata.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 19, 2026, Mzee Butiku alisema hafahamu mahali alipo Polepole kwa sasa, akisisitiza kuwa taarifa zinazomhusisha na suala hilo si za kweli.
Chanzo; Global Publishers