"Toka nimekaa matamko manane yametolewa na TEC lakini ukienda chini chini wenyewe kwa wenyewe wanapingana kwamba matamko hayafanyi kazi vizuri. Kwa sababu waliosimama kwenye mstari wa haki wanaona ile ni batili inayofanyika.
"Na hawaungani nao wanaona ni batili. Niseme kwamba Tanzania yetu ni nchi ya Umoja, ushikamano, amani na utulivu ndio ngao zetu. Tusivurugwe ndugu zangu kupitia milengo yetu ya dini, siasa na milengo yoyote ile hatupaswi kuivuruga nchi yetu kwamba aliyepo juu ya Serikali humtaki.
"Kuna muda hii ni nchi ya demokrasia. Kufanya makosa yake semeni. Kosa la Serikali ya Awamu ya Sita kueneza huduma za afya Tanzania hilo ni kosa letu? Shule nzuri mpaka Vijijini hilo ndio kosa letu? Au kukuza uchumi wa Tanzania? Kama humpendi anayeongoza stahimiri tu! - Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam.
Chanzo; Clouds Media