Jeshi la Polisi nchini limesema linaendelea kulinda usalama wa raia na mali zao, ili kuhakikisha wanaendelea na shughuli zao kama kawaida, huku likionya kama kuna ambaye atajitokeza na kukaidi kutii sheria za nchi kwa lengo la kuhatarısha usalama wa nchi na kusimamısha
shughuli za kiuchumi na kijamil zisiendelee kama wanavyo
hamasishana na kudanganyana, watawadhibiti ili nchi ibaki salama na Watanzania wema na wapenda amani wabaki salama.
Hayo yamebainishwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime, na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya shughuli zao na kufuata maelekezo watakayo kuwa wanapewa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama maeneo yote nchini na kutii sheria za nchi kwani hayo yote yanafanyika ili Taifa liendelee kuwa salama.
Chanzo; Bongo 5