Serikali imetoa taarifa ya kuachiliwa huru kwa vijana 1,736 kati ya 2,045 nchi nzima waliokuwa wakishikiliwa kwa kesi ya uhaini kufuatia agizo la Rais.
Katika taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Juma Zuberi Homera watuhumiwa wengine 309 bado wanaendelea kuchunguzwa, huku serikali ikisisitiza kuwa uchunguzi huo unafanyika kwa umakini ili kubaini ukweli bila kumuonea mtu yeyote.
Uamuzi unafanyika siku kadhaa tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipoagiza mahakama kupitia upya mashauri yote na kuwaachia wale ambao walijikuta wakishiriki maandamano kwa kutokujua, kufuata mkumbo, au bila dhamira ya kufanya uhalifu.
Aidha, Mamlaka zimeahidi uwazi katika hatua zote mpaka masuala yote yatakapokamilika.
Chanzo; Clouds Media