Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Uandikishaji Kupungua Mashuleni, Wataka Wanawake Wasitishe Uzazi wa Mpango

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe wamependekeza wanawake kuacha kutumia uzazi wa mpango wakidai hatua hiyo imechangia kupungua kwa idadi ya watoto, hali iliyosababisha kushuka kwa uandikishaji wa wanafunzi katika shule za awali na msingi wilayani humo.

Pendekezo hilo limetolewa mwishoni mwa wiki wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili na kupitisha rasimu ya bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe, ambapo suala la upungufu wa watoto walioandikishwa shule lilijadiliwa kwa kina.

Madiwani wamesema katika tathmini yao, elimu ya uzazi wa mpango imewafikia wananchi wengi na kusababisha kupungua kwa kasi ya uzazi, jambo linaloathiri idadi ya wanafunzi wanaojiunga na shule pamoja na mustakabali wa nguvu kazi ya baadaye wilayani humo.

Mmoja wa madiwani hao, Annaupendo Gombela wa Kata ya Mdandu, amesema Baraza la Madiwani limeona umuhimu wa kuhamasisha wanawake kuacha kutumia uzazi wa mpango ili kuongeza idadi ya watoto na nguvu kazi ya baadaye.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe, Agnetha Mpangile amesema kuna haja ya madiwani na viongozi wa jamii kukaa na wananchi ili kuhamasisha suala la uzazi.

 

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: