Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mmoja Auawa kwa Tuhuma za Ujambazi

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limethibitisha kuua mtu mmoja ambaye majina yake hayajatambulika, katika tukio la kudhibiti ujambazi ndani ya Ziwa Tanganyika, baada ya majambazi kuvamia wavuvi na kupora zana mbalimbali za uvuvi huku wengine wakielezwa kukimbia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Filemon Makungu amethibitisha tukio hilo, na kuongeza kuwa watuhumiwa walifuatiliwa na Polisi baada ya raia wema kutoa taarifa. Katika tukio hilo, majambazi walianza kufyatua risasi kabla ya majibizano kuanza na mtuhumiwa huyo kupigwa risasi na kufariki dunia.

Katika tukio hilo, vitu mbalimbali vimekamatwa ikiwemo silaha, risasi, mashine za wavuvi na nyavu za kuvulia. Kamanda Makungu amewataka wavuvi kufika kituo kikuu cha Polisi Kigoma ili kubaini mali zao. 

 

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: