Dar es Salaam. Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwanaharakati maarufu kwenye mitandao ya kijamii ya X na Instagram anayeishi Marekani, Mange Kimambi, umedai kuwa bado unaendelea na upelelezi.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Clemence Kato ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa kutajwa.
Kato ametoa taarifa hiyo leo, Alhamisi Desemba 4, 2025, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hassan Makube, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.
Chanzo; Mwananchi