Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Roli Lavamia Bodaboda, Wanne Wafariki

Watu wanne wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa katika ajali mbaya iliyotokea usiku wa kuamkia leo, Desemba 12, 2025, katika Mtaa wa Makulu jijini Dodoma, baada ya lori la mchanga aina ya Mende kupoteza mwelekeo.

Mashuhuda wamesema lori hilo, lililokuwa likitoka njia ya UDOM kuelekea katikati ya jiji, lilishindwa kukata kona katika mteremko wa eneo hilo baada ya mpira wa breki kupasuka na hivyo kuacha njia kabla ya kuwavamia madereva wa bodaboda waliokuwa wamepaki katika kituo hicho, pamoja na mteja aliyekuwa dukani.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabir Shekimweri, alifika eneo la tukio na kuthibitisha kuwa vijana watano wa bodaboda pamoja na pikipiki zao walipitiwa na lori hilo.

“Si tukio la kwanza kwenye eneo hili. Huu ukuta sasa ni takribani mara ya pili unajengwa baada ya kuharibiwa na ajali kama hizi, na hii ni kama ajali ya tatu kutokea katika eneo hili,” amesema Shekimweri.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti huku majeruhi wakipelekwa hospitalini kwa matibabu.

Vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na uchunguzi zaidi.

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: