Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Sababu za Maandamano Kukatazwa Disemba 9

Jeshi la Polisi limeyapiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika nchi nzima yasifanyike.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Ijumaa hii, imesema kulingana na ufuatiliaji wa kina waliofanywa na unaoendelea kufanywa kwenye Mitandao ya Kijamii na kwa watu mbalimbali na mbinu zinazohamasishwa zitumike kuanzia siku hiyo ya maandamano ya tarehe 9 Disemba 2025 kama ilivyoelezwa katika taarifa ya Jeshi la Polisi ya Disemba 3,2025 kuwa wanahamasishana kufanya yafuatayo;

1. Siku hiyo ya maandamano yasiyo na kikomo yaani tarehe 9 Disemba 2025
wanaelekezana ambaye hajui kutumia silaha na hajapitia mafunzo siku hiyo asishike silaha wawaachie waliopata mafunzo ya matumizi ya silaha.(Kwa maana rahisi watu hawa wanazo silaha za kutimiza lengo ambalo.

2. Kupitia mitandao na klabu mbalimbali za mtandaoni wanahamasishana
wahakikishe hakuna shughuli yoyote itakayokuwa inaendelea.

3. Pia wahakikishe wanaharibu na kuchoma moto minara yote ya mawasiliano ili nchi nzima ikose mawasiliano.

4. Wanahamasishana wahakikishe bandari ya Dar es Salaam haifanyi kazi
kwani watafunga barabara zote za kuingia na kutoka bandarini.

5. Siku hiyo na kuendelea wanahamasishana wafunge barabara zote za kuingia na kutoka katika mipaka yote ili kuhakikisha hakuna anayetoka au kuingia nchini.

kulingana na Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi inayotoa maelekezo na masharti ya kufanya, kukusanya, kuunda au kufanya mkusanyiko au maandamano na kutokana nal mbinu za kihalifu ambazo zimebainika
wakihamasishana kuzitumia kuanzia tarehe 9 Disemba 2025, Maandamano yanayopewa jina la maandamano ya amani na yasiyo na kikomo yamekosa sifa za kisheria za kuyaruhusu kufanyika.

 

Chanzo; Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: