Machafuko ya uchaguzi wa Oktoba 2025 nchini Tanzania yalifunikwa na giza zito la kuzimwa kwa intaneti, baada ya mrindimo wa bunduki kunyamaza ghafla. Sasa, ushahidi mpya unafichua kile ambacho hakikusimuliwa, vifo vya watu ambao idadi yao bado haijulikani, miili iliyotoweka, na tuhuma za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaodaiwa kufanywa na vyombo vya usalama. Kurunzi ya DW inamulika kilichotokea Mwanza, jiji la pili kwa ukubwa nchini Tanzania, na inakuja na undani ambao haujawahi kuwekwa hadharani.
Chanzo; Dw