Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Maiti Zaonekana Mtoni, Serikali Iingilie Kati

Wakazi wa mitaa ya Mruki na Msasani katika Halmashauri ya Mji wa Babati mkoani Manyara wameiomba Serikali kuwajengea daraja la kudumu katika Mto Fahhay ili kuondoa hatari inayowakabili wanafunzi takribani 200 wa Shule ya Msingi Shikizi ya Mruki, ambao hulazimika kuvuka mto huo kila siku kupitia daraja la mbao kwenda shuleni.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo, Bakari Said, amesema licha ya daraja hilo la mbao kuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi kwa zaidi ya miaka mitatu, kwa sasa limekuwa hatari kutokana na baadhi ya mbao na miti iliyotumika kuanza kuoza pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watumiaji.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mruki, Abdilahi Rajabu, amesema daraja hilo ni kiungo muhimu kinachounganisha mitaa ya Sinai na Mruki, ambapo asilimia kubwa ya watoto kutoka maeneo hayo wanasoma katika Shule ya Msingi Shikizi ya Mruki.

Aidha, wakazi wa eneo hilo wamesema wakati wa mvua kali mto huo hujaa maji na wakati mwingine maiti kutoka maeneo ya juu husombwa na maji kupita katika mto huo, jambo linaloongeza hofu na hatari kwa wanafunzi pamoja na wananchi wanaovuka kila siku.

Kutokana na hali hiyo, wakazi hao wameiomba Serikali kuingilia kati haraka kwa kujenga daraja la kudumu na salama ili kulinda maisha ya wanafunzi na wananchi wanaotumia njia hiyo.

 

 

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: