Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba ametangaza mwaka huu hakutakuwa na sherehe za maadhimisho ya uhuru wa Tanganyika Desemba 9, huku fedha zilizopangwa kwa shughuli hiyo zielekezwe kurekebisha miundombinu iliyoharibiwa katika vurugu za Oktoba 29.
“Desemba 9 hakutakuwa na sherehe za kuadhimisha hiyo Desemba 9 na gharama ya fedha ambazo zilikuwa zitumike kwenye sherehe (Rais Samia) ameelekeza ziende kutengeneza miundombinu hii iliyoharibika,” amesema.
Ametaka kuanzia leo, sekta zinazohusika zikae na kuanza kuratibu fedha zote zilizopangwa kwa ajili ya sherehe, zipelekwe haraka kurekebisha miundombinu iliyoathiriwa na vurugu za Oktoba 29, mwaka huu.
Dk Mwigulu ameyasema hayo leo Novemba 24, 2025 alipokuwa eneo la Mbezi kwa Yusuph wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam wakati akizungumza mbele ya wanananchi baada ya kufanya ziara kwenye vituo vya mwendokasi Barabara ya Kimara-Mbezi, kuangalia miundombinu iliyoathiriwa na vurugu za Oktoba 29, mwaka huu.
Chanzo; Mwananchi