Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wanajeshi 200 Wazuia Mapinduzi

Waziri wa mambo ya nje wa Benin amesema wanajeshi wapatao 200 wa Afrika Magharibi, wengi wao kutoka Nigeria na Ivory Coast, wako Benin kuiunga mkono serikali kufuatia mapinduzi yaliyoshindwa Jumapili.

Jaribio hilo lilishindwa baada ya Nigeria kutuma ndege za kivita kuwafukuza waasi kutoka kwenye kambi ya kijeshi na makao makuu ya televisheni ya serikali, ambapo walikuwa wametangaza kuchukua mamlaka.

Hii ni mara ya kwanza kwa maafisa kusema ni wanajeshi wangapi wa kigeni walitumwa nchini humo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Benin Olushegun Adjadi Bakari siku ya Alhamisi alisema baadhi ya wanajeshi wa kikanda waliotumwa wamebaki nchini "kama sehemu ya operesheni ya kusafisha."

Msako wa watu waliohusika katika mpango huo unaendelea, huku kiongozi wa mapinduzi yaliyoshindwa akidaiwa kukimbilia katika nchi jirani ya Togo.

Wanajeshi waasi walihalalisha matendo yao kwa kumkosoa Rais Patrice Talon, jinsi anavyoshughulikia "kuzorota kwa hali ya usalama kaskazini mwa Benin."

Jumuiya ya kikanda ya Afrika Magharibi, Ecowas, ilituma wanajeshi kutoka Nigeria, Ghana, Sierra Leone, na Ivory Coast ili kuvishikilia vituo muhimu na kuzuia vurugu.

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: