Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV, amesisitiza kwamba dini zina jukumu la kuepuka kutumia imani kuhalalisha vurugu au vita na badala yake kuwa nyumba za amani, ambapo uadui hushughulikiwa kupitia mazungumzo, haki na msamaha.
Papa Leo ameyasema hayo leo kupitia ujumbe wa kanisa linapoadhimisha Siku ya Amani Duniani Januari, mosi anazungumzia uzito wa wakati huu huku akipendekeza maono ya amani ambayo haina silaha, akipinga vurugu, na kuhamassisha uwazi wa kimaadili, mazungumzo na ubadilishaji wa mioyo.
Kiongozi huyo amesema ukweli huleta mabadiliko ya kudumu kwa wale wanaoupokea, akithibitisha kwamba amani ya Kikristo inafanya kazi na inavuruga katika kukataa vurugu.
“Jamii zinapopoteza mtazamo wa amani kama ukweli ulio hai. Hali ya mapambano inatawala siasa za kimataifa, na kudhoofisha diplomasia na sheria za kimataifa. Injili inaunganisha amani na kutokuwa na vurugu kisiasa na kijamii,” amesema Papa Leo.
Chanzo; Nipashe