Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Marekani, Rwanda Inahatarisha Amani Afrika Mashariki

Marekani, imeilaumu Rwanda kwa kuchochea vita vya kikanda, kwa kuliunga mkono kundi la waasi wa M23, mashariki mwa DRC.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya kusainiwa makubaliano ya amani yaliosimamiwa na Marekani.

Awali balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Mike Waltz, aliliambia Baraza la Usalama la Umoja huo kwamba, badala ya kupiga hatua kuelekea amani, Rwanda inaongoza eneo hilo kuelekea ukosefu wa utulivu na vita.

Pia amesema Marekani ina wasiwasi mkubwa na inazidi kukatishwa tamaa kwa kuzuka upya kwa ghasia Mashariki mwa Kongo.

Waltz anadai kuwa vikosi vya ulinzi vya Rwanda vimetoa msaada wa vifaa, mipangilio na mafunzo kwa M23 pamoja na kuisadia vitani. Hata hivyoRwanda imeendelea kukanusha kuliunga mkono kundi hilo la waasi.

 

Chanzo; Dw

 

 

Kuhusiana na mada hii: