Zambia inakabiliwa na mvutano huku Kanisa Katoliki na masharika ya kiraia yakijiandaa kuongoza maandamano ya kitaifa tarehe 28 Novemba kupinga mchakato wa marekebisho ya katiba. Wanasema mchakato huo ni kinyume cha sheria na unaoharakishwa na unazitenga sauti za raia.
Pia wanadai kwamba hauna msingi wa kutosha wa kisheria. Wakosoaji wanadai majadiliano hayakuwa ya kutosha na muda uliowekwa ni mchache sana, wakishuku mkono wa kisiasa kwa upande wa serikali. Viongozi wa kanisa wanaonya kwamba mageuzi haya yanaweza kuathiri masuala muhimu ya kitaifa na pengine kuwanufaisha walioko madarakani pekee. Wanataka mchakato huo uahirishwe hadi baada ya uchaguzi wa 2026. Serikali, wakati huo huo, imetoa onyo kuhusu maandamano yaliyopangwa.
Chanzo; Dw