Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Trump Aifungulia Bbc Kesi Ataka Matrilioni

Rais wa Marekani, Donald Trump, amefungua kesi dhidi ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), akidai fidia ya dola bilioni 5 (Sh12.35 trilioni) kwa madai ya kudhalilishwa (defamation) kufuatia uhariri wa hotuba yake ya Januari 6, 2021.

Kwa mujibu wa hati ya madai iliyowasilishwa katika Mahakama ya Shirikisho ya Wilaya ya Kusini ya Florida, Trump pia amefungua dai jingine tofauti la dola bilioni 5 (Sh12.35 trilioni) akidai BBC ilikiuka sheria za biashara za jimbo hilo. Hatua hiyo inaleta jumla ya madai ya fidia kufikia dola bilioni 10 (Sh25 trilioni) kwa hoja mbili za kesi hiyo.

Trump anadai BBC ilihariri hotuba yake ya Januari 6, 2021 kwa kuunganisha vipande viwili tofauti vya hotuba hiyo kwa lengo la kupotosha maana halisi ya kauli zake.

Hotuba hiyo ilitolewa kabla ya baadhi ya wafuasi wake kuvamia jengo la Bunge la Marekani (Capitol) wakati Bunge likijiandaa kuthibitisha ushindi wa Rais wa wakati huo, Joe Biden, katika uchaguzi wa 2020 ambao Trump aliendelea kudai, bila ushahidi, kuwa uliibiwa.

Hadi sasa, BBC haijatoa majibu rasmi kuhusu kesi hiyo, licha ya ombi la kutoa maoni kutoka Shirika la Habari la Associated Press (AP). Hata hivyo, mwezi uliopita, BBC iliomba radhi kwa Trump kuhusiana na uhariri wa hotuba hiyo, ingawa ilikanusha madai ya kumchafulia jina, hata baada ya Trump kutishia kuchukua hatua za kisheria.

Mwenyekiti wa BBC, Samir Shah, alitaja tukio hilo kama kosa la maamuzi hatua iliyosababisha kujiuzulu kwa mtendaji mkuu wa shirika hilo pamoja na mkuu wa idara ya habari.

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: