Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Bobi Wine Agoma Kujisalimisha

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, ametoa majibu makali akipinga agizo la mkuu wa majeshi ya nchi hiyo, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, lililotaka ajisalimishe kwa polisi ndani ya saa 48.

Katika taarifa aliyotoa Januari 20, Bobi Wine alitupilia mbali agizo hilo akilielezea kuwa ni njama ya vitisho na uonevu wa kisiasa.

Alisema hatokubali kuogopeshwa na kile alichokiita utawala wa kikatili, akiwatuhumu Jenerali Muhoozi na Rais Yoweri Museveni kwa kuhusika na njama za mara kwa mara za kutaka kumuua pamoja na ukandamizaji dhidi ya wafuasi wake.

“Ninakataa kuogopeshwa na utawala huu waoga,” alisema Bobi Wine, akisisitiza kuwa mapambano yake ni ya kudai haki, demokrasia na uhuru wa wananchi wa Uganda, si uasi kama inavyodaiwa na serikali.

Agizo hilo la kujisalimisha lilitolewa na Jenerali Muhoozi Kainerugaba kupitia matamshi yake ya umma, ambapo alionya kuwa endapo Bobi Wine hatatii, atachukuliwa kama “mtoroshi au mwasi.”

Kauli hiyo imezua mjadala mkubwa ndani na nje ya Uganda, huku wachambuzi wakieleza wasiwasi juu ya matumizi ya nguvu za kijeshi katika masuala ya kisiasa.

Hata hivyo, Muhoozi alisisitiza kuwa agizo hilo ni msimamo wake binafsi, akijaribu kumtenga baba yake, Rais Yoweri Museveni, na hatua hiyo.

Licha ya kauli hiyo, wapinzani na wanaharakati wa haki za binadamu wanaeleza kuwa ni vigumu kutenganisha kauli za mkuu wa majeshi na serikali inayotawala, hasa ikizingatiwa historia ya mvutano kati ya Bobi Wine na mamlaka.

Tukio hili linajiri wakati hali ya kisiasa nchini Uganda ikiwa tete, kufuatia madai ya ukandamizaji wa upinzani, kukamatwa kwa wanaharakati na matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji.

Jumuiya za kimataifa zimeendelea kutoa wito wa kuheshimiwa kwa haki za binadamu, utawala wa sheria na nafasi ya vyama vya upinzani kufanya siasa zao bila vitisho.

 

 

 

 

Chanzo Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: