Takribani watu 11, wakiwemo watoto watatu, wameuawa kwa kupigwa risasi katika baa moja iliyopo kwenye kitongoji cha Saulsville, magharibi mwa Pretoria, nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa za polisi, watu wengine 14 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini wakiwa na majeraha ya risasi. Tukio hilo lilitokea leo mapema katika baa isiyo na leseni, na limeibua taharuki kubwa katika eneo hilo.
Polisi wanaendelea kuwasaka wahusika wa shambulio hilo, na wamethibitisha umri wa watoto waliouawa kuwa ni mvulana wa miaka 3, mwingine miaka 12, na msichana mwenye miaka 16.
Afrika Kusini inaendelea kukabiliwa na viwango vya juu vya uhalifu, huku ikirekodi zaidi ya mauaji 26,000 mwaka 2024, sawa na wastani wa zaidi ya mauaji 70 kwa siku.
Chanzo; Global Publishers